November 23, 2020 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dr. Tulia Ackson amezungumza na Waandishi wa Habari nyumbani kwake na kuwaeleza ratiba yake kuwaona na kusikiliza hoja na kero za Wananchi ambapo amesema ratiba hiyo itakuwa mara mbili kwa kila wiki ikiwa ni siku ya Alhamis pamoja na Jumamosi.

“Tutakuwa na utaratibu wa kusikiliza Wananchi na kwa sababu Jimbo hili la Mbeya mjini ni kubwa na lina kata 36 kwahiyo tutakuwa na siku mbili kwa wiki kwa ajili ya kuwasikiliza Wananchi na tutakuwa na maeneo mawili tofauti, kwanza tutawasikiliza Wananchi katika eneo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya na siku itakuwa ni Alhamis na muda ni kuanzia saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni”-Dr. Tulia Ackson