WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza waendesha maghala kuacha kukata tozo ya upungufu wa uzito wa korosho ghafi zilizohifadhiwa ghalani (unyaufu) kwa wakulima na wanunuzi kwa kuwa tozo hiyo imeshaondolewa na suala hilo halijathibitishwa kitaalamu.

 

Ametoa agizo hilo leo (Jumamosi, Novemba 28, 2020) katika kikao kati yake na Wakuu wa Mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Ruvuma, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Kilimo, Viwanda na Biashara pamoja Mrajisi wa Ushirika. Kikao hicho kimefanyika kwenye  ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Mlimwa  jijini Dodoma