December 23, 2020 Mbunge wa Mbeya Mjini na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson kupitia taasisi yake ya Tulia Trust ametoa msaada wa mifuko 100 ya Cement katika Shule ya Sekondari Hayombo iliyopo kata ya Iganjo kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa madarasa unaoendelea katika shule hiyo.
Dr. Tulia amesema>>>”Tuendelee kushirikiana na Serikali katika kuboresha miundombinu ya elimu ili watoto wetu waweze kujisomea katika mazingira mazuri, hawa watoto tunaowajengea haya maeneo ndio tunaowatengeneza kuwa viongozi wetu wa baadae”
“Hayombo ni mojawapo ya Shule zinazofanya vizuri hapa Mbeya Jiji, kama mnavyofahamu Tulia Trust kila mwaka huwa tunatoa tuzo mbalimbali za elimu ikiwemo Shule bora, Walimu bora na Wanafunzi bora hivyo ni imani yangu mwaka 2021 Shule hii itachukua tuzo nyingi”- Dr. Tulia Ackson
“Siku ya leo Tulia Trust tumeleta mchango wa mifuko 100 ya cement kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa madarasa, huu ni mwendelezo tu na tutaendelea kushirikiana katika sehemu mbalimbali kwa lengo la kuongeza kasi ya maendeleo ya elimu ndani ya Jiji letu”- Dr. Tulia Ackson
“Tuliwaahidi tutafanya kazi na kazi tutaendelea nayo kwa ajili ya kuwasaidia Wananchi, Mbeya mjini mmeshampata Mbunge anayetuli Bungeni ambaye ni Tulia na ni Mbunge wa wote. Sisi wote ni ndugu na muda huu ni muda wa kufanya kazi kampeni zimeisha hivyo tusibaguane na badala yake tuendelee kufanya kazi kwa pamoja, Mimi ni mtumishi wenu na ni muwakilishi wenu”-Dr. Tulia Ackson
0 Comments
Post a Comment