Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akihutubia katika maadhimisho ya kilele cha Siku ya UKIMWI Duniani ambayo yamefanyika kimkoa Wilayani Mbarali.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Reuben Mfune akizungumza wakati wa Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika Kimkoa wilayani Mbarali.
Mbunge Vitimaalumu Mwakilishi wa Wanawake Taifa  Bahati Ndingo amepata fursa ya kutoa nasaha Siku ya UKIMWI Duniani Wilayani Mbarali.
Dkt Salum Manyata Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mbeya
Emmanuel Petro Mratibu Tume ya Kudhibiti Mkoa wa Mbeya
Hija Wazee Mkurugenzi Idara ya Jamii Watereed Tanzania
Stellah Kategile Ofisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mbeya
Maandamano Siku ya UKIMWI Duniani Viwanja vya Barafu Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.
Wasichana walio katika mpango wa Wasichana wa DREAM wakishiriki katika Maandamano ya Siku ya UKIMWI Duniani Viwanja vya Barafu Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akiwa na baadhi ya Viongozi wa serikali wa Mkoa wakipokea Maandamano ya Siku ya UKIMWI Duniani Viwanja vya Barafu Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.
Baadhi ya washiriki kwenye Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani wakiwasha mishumaa kuashiria kumbukumbu kwa watu waliofariki kwa ugonjwa wa UKIMWI Duniani.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Mbarali Mrakibu wa Polisi Janeth Masangano akizungumza na wananchi wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha Siku ya UKIMWI Duniani Viwanja Vya Barafu Rujewa Wilayani Mbarali.



Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akipata Maelezo kwenye Banda la Wasichana walio katika Mpango wa DREAM namna ambavyo wamejiwezesha katika shughuli mbalimbali za ujasiriamali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila akipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa SHDEPHA Wilayani Mbarali Francis James alipotembelea Banda la SHDEPHA kwenye maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yaliyofanyika Kimkoa Viwanja vya Barafu Rujewa Wilayani Mbarali.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila alipotembelea Banda la Dawati la Jinsia la Polisi wakati wa Maadhimisho ya  Siku ya UKIMWI Duniani Viwanja vya Barafu Rujewa Wilayani Mbarali.
Baadhi ya Wakazi wa Rujewa wakiwa katika foleni kwenye hema kwa ajili ya kupima Afya wakati wa Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani.
Mkurugenzi wa Jamii wa Watereed Tanzania Hija Wazee akitoa maelezo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila Siku ya UKIMWI Duniani kwenye Viwanja vya Barafu Rujewa Wilaya ya Mbarali.
Vijana wa Taasisi ya Mikopo na Wawezeshaji Wajasiriamali ya Tulia Trust wakishriki katika Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani kwenye Viwanja vya Barafu Rujewa Wilayani Mbarali.


Uwashaji wa Mishumaa Siku ya UKIMWI Duniani
Wasichana walio katika mpango wa DREAM wakishiriki maonesho ya siku ya UKIMWI Duniani Viwanja vya Barafu Rujewa Mbarali.
Baadhi ya Wanafunzi wa shule ya Sekondari Rujewa wakishiriki Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani Viwanja vya Barafu Rujewa Mbarali.

 MAADHIMISHO YA SIKU YA UKIMWI DUNIANI MBEYA YAFANYIKA KIMKOA WILAYANI MBARALI.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amewakata wakazi wa Mkoa wa Mbeya kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa ukimwi kutokana na ugonjwa huo kuendelea kukua mkoani humo.

Akizungumza kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya UKIMWI Duniani ambayo yamefanyika kimkoa wilayani Mbarali Chalamila kukua kwa ugonjwa wa UKIMWI kunapunguza kasi ya nguvu kazi ya Taifa nchini.

Amesema maambukizi katika mkoa wa Mbeya ni asilimia 9.4 ambayo ni chini ya maambukizi ya kitaifa ya asilimia 4.5 na kwamba ni muhimu kwa wakazi wa mkoa huu kuendelea kuchukua tahadhari.

Amesema ni vigumu kuamini kwamba matumizi ya kinga dhidi ya ugonjwa UKIMWI ikiwemo matumizi ya mipira ya kiume yanafuatwa kutokana ukweli kuwa bado hakuna dalili za kupungua kwa ugonjwa huo katika mkoa wa Mbeya.

‘’Nitoe wito kwa wakazi wa Mbeya, tuishi kwa kujizatiti vizuri kuepuka maambukizi mapya. Tufike hatua za kulichukulia suala hili ni jambo maalumu litakalosaidia kupunguza maambukizi ya ugonjwa huu’’amesema Chalamila.

Awali  Mkurugenzi wa Idara ya jamii kutoka Mradi wa WaterReed Tanzania Hija Wazee amesema katika maadhimisho hayo taasisi ya Watereed imetoa huduma za tohara upimaji wa maambukizi ya UKIMWI katika wilaya ya Mbarali ikiwa ni mpango wa mradi huo kufikia asilimia sifuri ya maambukizi hayo nchini.

Amesema katika kuhakikisha huduma za maambukizi ya UKIMWI inazidi kupungua Taasisi ya Watereed kwa kushirikiana na taasisi nyingine za PACT, HJFMRI zimewakusanya wasichana walio nje ya shule kwenye mradi maalumu wa DREAM ambao wasichana zaidi ya 350 wenye umri wa miaka 15-24 unawawezesha wasichana hao kujitambua na kutojiingiza katika maambukizi ya UKIMWI.