*Naibu amtaka mkandarasi wa Miradi wa maji Arusha kuongeza kasi.*

Mhandisi Maryprisca Mahundi, Naibu Waziri wa Maji amekagua mradi wa Maji Arusha ambao unatekelezwa kwa gharama ya shilingi bilioni 520. Mhe. Naibu Waziri ameridhishwa na ubora wa mradi. Hata hivyo amemtaka mkandarasi kuongeza kasi ili mradi huo ukamilike haraka.

Amesema mkataba wa utekelezaji wa mradi unaelekeza mradi kukamilika Agosti mwaka 2021 lakini mkandarasi anapaswa kuhakikisha mradi unakamilika Mwezi Mei mwakani kwani itampunguzia muda wa kufuatilia huku ukitoa fursa kwa wananchi kuianza kupata huduma ya majisafi.

Amesema nia ya serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata Huduma ya majisafi na Salama karibu na maeneo yao. Hivyo viongozi wanajukumu la kuhakikisha suala hilo linafanikiwa.

Ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na Salama jijini Arusha (AUWASA) kwa kusimamiwa vizuri huku akiwataka wahakikishe maeneo unakopita mradi yanaachiwa matoleo ya kusambaziwa huduma hiyo.

Kuhusu ujenzi wa miundombinu ya majitaka amewataka viongozi wa AUWASA kutoa elimu kwa Wananchi namna wanavyoweza kunufaika na mradi huo kwa kuelekeza miundombinu ya ujenzi wa nyumba zao kwenye mifumo hiyo.