NHIF YAJA NA MACHINGA AFYA.
Na Ripota wa Mbeya Yetu.
Mfuko wa Taifa Bima ya Afya NHIF katika mkakati wake wa kuwafikia Watanzania wengi ulianzisha mpango maalumu kwa Wafanyabiashara ndogondogo maarufu "Wamachinga", mpango wa MACHINGA AFYA ili kulisaidia kundi hilo maalumu katika jamii.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF Mkoa wa Mbeya, Mbala Shitindi, leo amekutana na kundi la Wamachinga wa Soko la Airport ya zamani na kutoa elimu kwa Wamachinga ili waweze kujiunga na mfuko kupitia Umoja wao.
"Huu ni mpango maalumu kusaidia makundi katika jamii kupata matibabu kwa Mfuko wa Bima ya Afya" amesema Shitindi.
Amefafanua kuwa kundi linapaswa kuwa na watu wasiopungua 100 ambao wanapaswa kuchangia kiasi cha Shilingi Laki Moja kwa kila mmoja ambao umeenda kuwakomboa kuepuka gharama za matibabu, kwani baadhi yao wamekuwa wakipoteza mitaji ya biashara kugharamia matibabu .
Shitindi amesema kuwa kwa gharama hizo mteja atanufaika kwa kupata huduma za matibabu katika vituo vyote vlivyosajiliwa kutoa huduma kwa Wanachama wa Mfuko wa Taifa NHIF nchini.
"Kupitia Mpango huu wataweza kuwasajili watoto wao kwa gharama ya Shilingi 50.400 kwa mwaka kwa kila mtoto mmoja" amesema Shitindi.
Nae Mwnyekiti wa Machinga Mbeya, Shadrack Mwamwenda amewataka kutumia fursa hizo zinazotelewa na Serkali kuboresha maisha yao kwa kuwa na uhakika wa matibabu na kulinda mitaji yao dhidi ya gharama za matibabu.
0 Comments
Post a Comment