Naibu waziri wa maji Mhandisi Maryprisca mahundi
Serikali kutumia Bilioni 34 kutekeleza mradi wa kutoa maji ziwa Chala.
Serikali imeahidi kutumia zaidi ya Sh Bil 34 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa kutoa maji ziwa Chala lililopo mpakani baina ya Tanzania na Kenya ili kuhudumia wananchi wa wilaya ya Rombo na maeneo jirani.
Mradi huo ambao upo katika hatua za mwisho baada ya kufanyiwa upembuzi yakinifu, utaondoa tatizo la maji safi na salama kwa wakazi wa wilaya hiyo ambao kwa sasa wanapata huduma ya maji kupitia kampuni ya Kiliwater ambayo imeanza kubadilishwa na kuwa Mamlaka ya Maji.
Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi (MB) amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kisale-Msaranga wilayani Rombo huku akiwahakikishia kuwa tatizo la maji litamalizika.
“Niwahakikishie wananchi wa Kisale. Tatizo la maji kijijini hapa litakuwa historia mara tu mradi huo utakapokamilika.”
Amesema hadi kufikia Mwishoni mwa mwezi Januari, 2021 Takribani Sh Bil 2 zitatumika kwa ajili ya mradi huo ambao upembuzi yakinifu umekamilika.
0 Comments
Post a Comment