Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt Tulia Ackson akishiriki kusafisha mitaro katika maeneo mbalimbali ya mitaa ya Kata ya Iyunga.





 Januari 9.2020:MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini leo ameshiriki kuzibua mitaro katika maeneo mbalimbali ya mitaa ya kata ya Iyunga Jijini Mbeya ambako mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha mifereji na mkitaro hiyo kuziba.

Dkt Tulia ambaye pia ni Naibu Spika wa Bunge (JMT) ameshiriki zoezi hilo la usafi pamoja na wakazi wa maeneo hayo majira ya asubuhi ambako baadhi ya maeneo yamekumbwa na mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Jijini Mbeya.