WAKAZI KATA YA KILAKALA MORO WAHAMASISHWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUTATUA KERO
16.01.2021.Afisa
Mtendaji Kata ya Kilakala Manispaa ya Morogoro Bi Amina Said Mhina akifafanua
jambo katika mkutano uliowahusisha baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kigurunyembe Kata
hiyo wakati wa kusikiliza kero za wananchi wa kata hiyo,(kulia) ni Diwani wa
Kata ya Kilakala Mh. Marco Mathias Kanga.
Akizungumza
katika Mkutano huo Bi Amina amewataka wananchi kujitokeza kwenye shughuli
mbalimbali za maendeleo na kueleza kuwa matatizo makubwa yanayohusiana na
uboreshaji wa miundo mbinu yatatatuliwa kwa ushirikiano wa serikali na
wananchi.
Aidha
amewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali hususani katika kipindi
hiki ambacho wanafunzi wa kidato cha
kwanza wanatakiwa kujiunga na masomo ya sekondari.
Naye Diwani
wa Kata hiyo Marco Kanga amesisitiza kwa kuwataka wakazi wa kata hiyo kuitikia
wito wa kujitokeza kwenye mikutano na shughuli za maendeleo ambako pia watapata
fursa ya kutoa kero na madukuduku yao.
0 Comments
Post a Comment