Buriani Baba, Kwaheri Kiongozi Wetu Kwa heri shujaa wetu, ndivyo anavyoonekana kusema katika moyo wake, Mbunge wa Jimbo la Lupa Mheshimiwa Masache Kasaka wakati akitia saini kitabu cha Maombolezo ya Hayati Dkt John Magufuli Bungeni Dodoma leo asubuhi.

 

Mheshimiwa Masache ameungana na wabunge wengine kuuaga mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ambaye mwili wake umefikishwa bungeni na wabunge kutoa heshima zao.

Mbunge huyo wa Lupa amemuelezea Hayati Magufuli kuwa alikuwa kiongozi shupavu aliyeongoza Taifa kwa ujasiri na Uthubutu ambaye alionesha mapenzi yake dhahiri kwa Watanzania.



Nenda JPM Nenda!! Tutaonana Baadaye