MHANDISI MARYPRISCA AWAFUTA MACHOZI MAHABUSU NA WAFUNGWA WANAWAKE GEREZA LA RUANDA MBEYA

Hatimaye machozi ya Mahabusu na Wafungwa wanawake wapatao 38 na Mtoto mmoja waliopo katika gereza la Mahabusu la Ruanda Jijini Mbeya yaanza  kufutwa.

Mahabusu hao walitoa kilio chao mbele ya Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi aliyeambatana na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Dkt Tulia Ackson ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani.

Kilio cha Mahabusu mbele ya Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ilikuwa ni pamoja na nafasi finyu ya Mabweni ya kulala sanjari na huduma za kijamii ambazo Mahabusu hao hujitegemea kwa kuuza bidhaa mbalimbali wanazotengeneza kwa mikono yao.

Akizungumza jana mara baada ya kutembelea gereza la Mahabusu Wanawake la Ruanda, Mhandisi Maryprisca aliahidi kutatua baadhi ya changamoto ikiwa ni pamoja na kununua magodoro 10 kwa ajili ya Mahabusu na Wafungwa gerezani hapo.

Akishukuru baada ya kupokea msaada huo wa magodoro 10 kutoka kwa Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi Mkuu wa gereza la Mahabusu Wanawake Mrakibu Mwandamizi wa Magareza Rehema Mwailunga amewataka wadau wengine kujitolea kwa moyo kusaidia mahitaji ya mahabusu na wafungwa wa gereza hilo.