Naibu Waziri wa Maji na Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kushirikiana na Madiwani  Viti Maalum Jiji la Mbeya wametoa mifuko  ya saruji kwa shule  Sekondari Mponja Jijini Mbeya kwa ajili ya ujenzi wa matundu kumi na mbili vyoo vya wasichana katika shule hiyo.

Akipokea saruji hiyo kutoka kwa Madiwani Viti Maalum Jiji la Mbeya Diwani wa Kata ya Igawilo Anna Ndidi amewashukuru Madiwani na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya kwani bado wana uhitaji mkubwa wa matundu ya vyoo.

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Shule ya Mponja Festus Abel Sawalla mbali ya kuwashukuru Madiwani  Viti Maalum Jiji la Mbeya na Mbunge Viti Maalum ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji amesema msaada huo umekuja kwa wakati kwani wana uhaba mkubwa wa matundu ya vyoo katika shule yao.