WALTER REED TANZANIA (WRP-T) YAKABIDHI KOMPYUTA,KAMERA NA TV KWA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA KWA JESHI LA POLISI MIKOA NYANDA ZA JUU.
Na Mwandishi Wetu, Mbeya
Jeshi la Polisi mikoa ya Mbeya,Songwe,Rukwa na Katavi limekabidhiwa Kompyuta, Kamera na Tv kwa ajili ya kusaidia mapambano dhidi ya Ukatili wa Kijinsia kwenye Madawati ya Polisi kutoka Taasisi ya HJFMRI-Walterreed ikiwa ni sehemu ya mapambano dhidi ya ukatili wa Kijinsia.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa HJFMRI Sally Chalamila na Katibu Mtendaji David Maganga, ikiwa ni sehemu ya kukamilisha siku 16 za ukatili kwa Kijinsia Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kijamii wa Taasisi ya HJFMRI-Walterreed Hijja Wazee amesema vifaa hivyo vimelenga kusaidia kwenye mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.
Amesema vifaa hivyo vitasaidia katika kuchukua ushahidi wa
matukio wanayokumbana nayo vijana wanaokumbana na ukatili wa kijinsia na kuweka
kumbukumbu sahihi katika mapambano hayo ambayo yanakwenda sanjari na
mapambano dhidi ya Maambukizi ya UKIMWI.
Kwa upande kwake Mratibu wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS)Mkoa wa Mbeya Emmanuel Petro amesema HJFMRI wamekuwa bega kwa bega serikali katika kupunguza ukatili wa kijinsia ambao pia ndio unaochochea maambukizi ya UKIMWI.
Petro amebainisha kuwa mapambano dhidi ya UKIMWI yanahitaji
sapoti kubwa kutoka kwa wadau na kwamba vifaa vilivyotolewa kwa Jeshi la Polisi
vitasaidia kuwepo kwa kumbukumbu kwa matukio mbalimbali ya Ukatili wa Kijinsia.
Akizungumza mara baada ya kupokea vifaa hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema kuwa msaada unaotolewa na Taasisi ya HJFMRI mara kwa mara kwa Jeshi la Polisi imechangia kwa sehemu kubwa kusaidia mapambano dhidi ya ukatili wa Kijinsia.
Kamanda Matei amesema kwa niaba ya Inspekta Generali wa Polisi Simon Sirro ametuma salamu za shukrani kwa HJFMRI kwa msaada wa vifaa ambavyo ni Kompyuta 4, kompyuta mpakato 2, Kamera 6,Tablet 2 na TV FLAT 1 na DVD Player 1.
0 Comments
Post a Comment