Naibu Waziri wa Maji Mhe. Maryprisca Mahundi (Mb) akiongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa kwanza wa Baraza la Mawaziri Kamisheni ya Bonde la mto Songwe. Mhe. Mahundi ni mwenyekiti mwenza katika mkutano huo, unaojadili masuala ya rasilimali za maji katika bonde la mto Songwe, ikihusisha nchi za Tanzania na Malawi.