Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandishi Anthony Sanga amezindua miongozo mitatu inayolenga kuwezesha na kurahisissha utendaji kazi katika Mamlaka za Maji nchini. Miongozo hiyo ni Muongozo wa Kuandaa Mkakati wa Kupunguza Upotevu wa Maji, Muongozo wa Usimamizi wa Dira za Maji na Muongozo wa Uendeshaji wa Mamlaka za Maji.
Katika hafla hiyo fupi iliyoandaliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) jijini Dar es salaam.
Mhandishbi Sanga amesisitiza utendaji kazi mzuri ili kuhakikisha adhma ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani inatimia.
Amesema Rais Samia ameonesha nia ya dhati ya kutatua changamoto za upatikananaji wa huduma ya maji kwa watanzania hivyo watumishi wa Wizara wana jukumu la kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao.
Aidha, katika hafla hiyo Mhandisi Sanga amekabidhi zawadi za vyeti na ngao kwa Mamlaka za Maji ambazo zimefanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao katika maeneo tofautitofauti. Vilevile amewapongeza EWURA kwa kuweka utaratibu wa kutoa zawadi Mamlaka za Maji za maji ambazo zimefanya kazi katika utekelezaji wa majukumu yao.







0 Comments
Post a Comment