Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca amewataka wanawake kutimiza wajibu wao katika ndoa.

Mahundi ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya wanawake Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mbeya.

Aidha amewataka wanawake kuwa wavumilivu na kuishi katika ndoto zao ili kuyafikia malengo yao.

Hata hivyo amewataka wanawake kufanya mambo yao kwa ufanisi zaidi badala ya kufanya kwa kuiga hivyo kushindwa kukidhi matakwa kwa kuwa sicho alichotarajia kukifanya.

Awali wanawake wamejengewa uwezo wa kuzijua haki zao za kisheria ili kuepuka manyanyaso katika ndoa pia masuala ya mirathi elimu ambayo imetolewa na Hakimu Mkazi Wilaya ya Mbeya.