Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Jumanne Mtambalike amesema lengo la mafunzo hayo ni kuvijengea uwezo vyombo vya habari ili viwe na mpango mkakati wa kuwa na vyanzo vipya vya mapato kwa njia ya kiteknolojia.
SAHARA VENTURES YAKUTANISHA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA MIKOA 11,WAJENGEWA UWEZO JUU YA MABADILIKO YA KITEKNOLOJIA.
KAMPUNI ya Sahara Ventures inayojihusisha na kujengea uwezo kwenye nyanja za Ubunifu, Ujasiriamali na Teknolojia kupitia miradi wake wa Swichi imetoa mafunzo kwa wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka mikoa 11 kuwajengea uwezo kupata vyanzo vipya vya mapato kupitia mabadiliko ya kiteknolojia.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Jumanne Mtambalike amesema lengo la mafunzo hayo ni kuvijengea uwezo vyombo vya habari ili viwe na mpango mkakati wa kuwa na vyanzo vipya vya mapato kwa njia ya kiteknolojia.
Kwa upande wao baadhi ya wawakilishi na wasimamizi wa vituo, wameelezea tija na mafanikio yatokanayo na mafunzo hayo kuelekea kwenye mabadiliko ya mfumo wa teknolojia.
Meneja wa mradi wa Swichi Angel Adam Kobelo ameuelezea mradi huo ambao uko chini ya kampuni ya Sahara Ventures na ufadhilii wa DW Academy,TMF na Aghakhan University umewakutanisha Wawakilishi wa vyombo vya habari kutoka mikoa 11 ambao wanajengewa uwezo kwa siku 5 jijini Dar es Salaam ili wamudu kukimbizana na mabadiliko ya kiteknolojia na kujiongezea mapato.
0 Comments
Post a Comment