MASACHE ASHIRIKI KIKAO CHA WADAU WA TUMBAKU DODOMA
Mbunge wa Jimbo la Lupa, Chunya Mhe.Masache Kasaka leo tarehe 13/04/2022 ameshiriki kikao cha Wadau wa Tumbaku, kinachofanyika Dodoma. Ameyaomba Makampuni ya Ununuzi wa Tumbaku nchi kuwaangalia kwa huruma wakulima kwenye msimu wa masoko ya tumbaku kutokana na changamoto ya mbolea kupanda bei ilihali bei ya tumbaku ipo chini. Aidha ameendelea kuiomba serikali iweze kusimamia madai ya malipo ya wakulima ya zaidi ya TZS 500,000,000 kutoka kampuni ya Grand Tobacco Limited ambayo ilinunua tumbaku wilayani Chunya mwaka 2020.



0 Comments
Post a Comment