Tatizo la Konde ni uaskofu na siyo Kuhamisha Dayosisi.
Kyela
ASKOFU wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Konde Dk Edward Mwaikali amesema mgogoro unaendelea ndani ya Dayosisi yake ni nafasi ya uongozi uaskofu na siyo kuhamisha makao makuu ya Dayosisi kutoka Tukuyu kwenda Usharika wa Ruanda Mbeya Mjini kama ilivyoonekana awali.
Dk Mwaikali alisema hayo jana wakati akizungumza katika ibada takatifu kwa waumini wa kanisa hilo usharika Kyela Mjini na kwamba mgogoro wa kuhamisha makao makuu ya Dayosisi kutoka Tukuyu kwenda jijini Mbeya ni kiini macho.
Alisema kilichofanyika Machi 28 mwaka huu Ushirika wa Uyole katika Mkutano mkuu wa dharula ulioitishwa na Mkuu wa kanisa KKKT Dk Fredrick Shoo na kufanya uchaguzi uliompitisha Geofrey Mwakihaba kuwa askofu mteule kimedhiirisha kuwa tatizo halikuwa kuhamisha Dayosisi bali cheo cha Uaskofu.
Mwakihaba aliwai kuwa Msaidizi wa Askofu DK Mwaikali kabla ya hajavuliwa nafasi ya utumishi na katibu Mkuu wa Dayosisi Agast Mwaka jana baada kuwageuke wenzake juu ya uamuzi wa kuhamisha Dayosisi ilhali alikuwa ni moja ya wajumbe walioshiriki kufanyaa maamuzi hayo.
Akizungumza na mamia ya waumini walioshirika ibada hiyo takatifu Dk Mwaikali alisema inasikitisha kuona watumishi wa Mungu kuwa wachonganisha na kuwavuruga watu badala ya kuwa daraja la kuwaunganisha.
"Ndugu yangu poleni kwa yote lakini yanapita jambo la kusikitisha watumishi wa mungu wamekuwa wafitini badala ya kuwa daraja la kuwaunganisha watu wao wamegeuka na kuwatenganisha " alisema Dk Mwaikali
Askofu Dk Mwaikali alisemaa waumini,wainjilisti na wachungaji ni vema wakatambua kuwa wanakazi kubwa ya kuhubiri neno la Mungu kwani vyeo walivyo navyo vinapita hivyo wanapaswa kusimama katika imani na neema ya Mungu itawawezesha kuwa na msimamo wa kusimamia kweli
"Kinacho tugombanisha ni nafasi ya uaskofu na si kuhamisha Dayosisi na hili nimelijua baada ya ule mkutano dharura uliofanyika Uyole nawambie katika hili ipo siku ukweli utajulikana na mambo yatakuwa bayana "alisema
Aidha Dk Mwaikali aliwasii waumini wa kanisa hilo Usharika wa Kyela Mjini na Dayosisi ya Konde kuendelea kusali na kuomba toba katika kipindi cha Kwaresma ambapo kanisa linapitia kipindi kigumu lakini wanaamini Mungu atawavusha salamaa na kulinda heshima zao kwani wanapaswa kuelewa kuwa kuna maisha baada ya Mgogoro kwisha.
Katika hatua nyingine Dk Mwaikali alisema anasikitishwa kuona wachungaji wamejiingiza katika Mgogoro huo na kuacha kazi ya kuchunga kondoo waliopewa na Mungu.
Alisema ni vema wachanguji hao wakaacha kujiingiza katika mgogoro na wajikite katika kazi ya kuchunga kondoo wa bwana hasa katika kipindi hiki cha kwaresma ambapo ni kipindi cha kufanya toba.
"Nimesikitishwa na wachungaji wetu wameacha kuwahudumia kondoo wa bwana katika kipingi cha kwaresma pasaka nao wamekomaa na mgogoro ambao halisaidii kanisa zaidi ya kuligawa" alisema
Akizungumzia kuvuliwa nafasi ya Uaskofu Dk Mwaikali alisema kuwa yeye bado na Askofu na kwamba barua iliyoandikiwa na Katibu wa KKKT ni uwongo na kwamba tatizo litaishi hivi karibuni kwana baraza maaskofu litaketi Mei 4 mwaka huu na kwamba katika Kikao cha Dodoma sauala la Konde halikujadiliwa kabisa ni vema waumini wakawa watulivu.
Mwishoo
0 Comments
Post a Comment