*VIGOGO CCM WASHIKANA MASHATI, TUHUMA NZITO ZA UPIGAJI WA FEDHA ZAIBUKA, SAHIHI YAGUSHIWA.*
*Na Laudence Simkonda-Momba*
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Momba mkoani Songwe Ndugu Hassain Nyalile ameibuka na kumtumuhu katibu mtendaji wa CCM wilaya ya Momba Ndugu Steven Shija kwamba amegushi sahihi yake na kwenda kuchota fedha za chama benki kiasi cha chilingi milioni 38.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Katika Ofisi za CCM wilaya ya Momba, zilizopo mji wa Tunduma, Nyalile amesema, Katibu wake wa Chama hicho amegushi sahihi yake na kwenda kutoa fedha benki ya NMB katika vipindi tofautitofauti.
“Ninayo Bank statement hapa, inaonyesha mimi nimehusika kutoa hizi fedha jambo ambalo, sikuwahi kushiriki utoaji wa fedha hizi, kwa maana hiyo amegushi sahihi yangu, na hili sitavumliana nitaomba vyombo vya uchunguzi viingilie kati hapa, maana huku ni kuchafuana bure” Nyalile.
Nyalile ametoa thuma nyingi kwa katibu huyo, ikiwa ni pamoja tangu aanze kufanya kazi katika wilaya hiyo, amekuwa haelewani na viongozi wenzake, huku akitumia vibaya mamlaka yake kuwagawa wanachama.
Akizungumza name kwa njia ya simu, katibu wa CCM Wilaya ya Momba Ndugu Steven Shija, amesema tuhuma hizo siyo za kweli, na kudai kuwa mambo hayo tayari yamezungumzwa kwenye vikao halali vya kichama na yalikwisha.
“Haya yanaibuka kwasabu tu mimi naonekana ni mwiba, wakati naingia pale nilita mambo hayaeleweki, kulikuwa na upigaji sana wa fedha, lakini nimefika nimeziba mianya ya matumizi yasiyoeleweka ya fedha, ndiyo matokeo hayo ya kuanza kushambuliwa mitandaoni, nikwambie tu mwandishi wewe fuatilia benki ukajilidhishe je hicho kinachosemwa ni kweli, maana hakuna benki inaweza kukubali kutoa fedha bila kuwepo kwa watia saini wote” Shija.
Shija amesema CCM wilaya ya Momba kwa sasa ipo imara zaidi ya jana, tofauti na madai ya katibu mwenezi kwamba eti chama kimepalaganyika, na kumalizia kuwa hiki ni kipindi cha uchaguzi yataibuka mengi zaidi ya hayo.
*Mwisho.*
0 Comments
Post a Comment