TIMU ya watendaji 15 kutoka Wizara ya Maji imefanya ziara ya siku 6 Nchini Afrika Kusini na Zimbabwe yenye lengo la kujifunza miradi mbalimbali kwa ajili ya kuboresha huduma za maji maeneo ya vijijini nchini Tanzania

Akizungumza kwa njia ya simu wakiwa mjini Pretoria nchini Afrika Kusini Naibu Waziri wa Maji amesema kwenye ziara hiyo wameambatana na Watendaji, Wahandisi,Wahasibu,Maafisa Ugavi na Maafisa Maendeleo ya jamii.



Amesema ziara ya timu hiyo imelenga kupata mafunzo kwa watendaji hao kutokana na adha wanayokumbana nayo wananchi ya upatikanaji maji umbali mrefu vijijini sanjari na kuondokana na tatizo la mashine za kusukumwa kwa dizeli ili kutumia mashine za umeme wa jua.





Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema ziara yao itachukua  siku sita nchini Afrika Kusini na baadaye nchini Zimbabwe ambazo ni ziara za kimafunzo kuona namna ya kupeleka huduma ya maji kwa gharama nafuu Pre-Paid Meters.