WIZARA YA MAJI YASHIRIKI KWENYE SEMINA MAALUMU YA MAPAMBANO YA UGONJWA WA KUPINDUPINDU.
29.08.2022. Wizara ya Maji imeshiriki katika semina maalumu Jijini Dar es Salaam katika mapambano dhidi ya Ugonjwa wa Kipindupindu.
Akizungumza ushiriki wa Wizara ya Maji katika semina hiyo, Naibu Waziri wa Maji Eng.Maryprisca Mahundi amesema Wizara ya maji imeshirikiana na Wizara ya Afya ili kuhakikisha ugonjwa wa Kipindupindu unatokomea.
"Tunawahikishia Wananchi upatikanaji wa maji safi na salama katika kipindi hiki cha mapambano ya Kipindupindu" amesema Eng Maryprisca.
Amefafanua kuwa Wizara ya Maji inaendeleza Kauli Mbiu ya Rais ya Kumtua Ndoo Mama Kichwani sanjari na kutoa elimu kwa jamii, watu waweze kunawa maji safi yanayotiririka kwa sabuni.
"Tunatoa huduma ya maji safi na salama lakini tunasisitiza matumizi sahihi ya maji safi na salama maeneo yote ya mikusanyiko" amefafanua Eng.Maryprisca.
Kadhalika Eng.Maryprisca amebainisha kuwa Wizara ya Maji imejiwekea mikakati kuhakikisha maeneo yote ya mikusanyiko kama vile mashuleni,Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali kunakuwa na maji kutosha na vyombo maalumu vya kuhifadhia maji ya kunawa.
Ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wananawa maji safi na salama yanayotiririka na kuepuka kunawa maji watu wengi kwa kutumia chombo kimoja.
0 Comments
Post a Comment