Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Mwajabu Mkomola akifungua mafunzo kwa Watendaji wa Biashara na Afya Mkoa wa Mbeya mafunzo yaliyoandaliwa na TBS
Meneja wa TBS Kanda ya Nyanda za Juu Abel Mwakasonda akitoa utambulisho kwenye mafunzo
Dkt Ashura Katunzi Kilewela akizungumza na washiriki kwenye mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji 
Afisa Biasara Mkoa wa Mbeya Richard Musingi Salegote akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wasiriki wa mafunzo

Washiriki wa mafunzo kutoka Halmashauri mbalimbali wakifuatila mafunzo

Viongozi mbalimbali kutoka TBS na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja katika mafunzo yaliyoandaliwa na TBS


TBS YATOA MAFUNZO WATENDAJI WA HALMASHAURI ZOTE MKOANI MBEYA

Shirika la Viwango Tanzania(TBS)limeendesha mafunzo kwa Watendaji vitengo vya Afya na Biashara Halmashauri zote nchini ambapo Mkoani Mbeya jumla ya washiriki ishirini wamepatiwa mafunzo hayo yenye lengo la kuwajengea uwezo hasa baada ya mabadiliko ya sheria mpya mgeni katika ufunguzi akiwa ni Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Mwajabu Mkomola.

Awali Meneja TBS Kanda ya Nyanda za Juu Abel Mwakasonda amewataka washiriki kuyazingatia mafunzo waliyoyapata ili wafanye kazi kwa uweledi na udalifu mkubwa ambapo amesema mafunzo yamewashirikisha maafisa Afya na Biashara kutoka Mbeya Jiji,Mbeya Vijijini,Kyela,Rungwe,Mbarali,Chunya na Busokelo.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TBS Dkt Ashura Katunzi Kilewela amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo washiriki waweze kuzijua sheria mpya,namna ya kuandaa viwango,kuhakiki ubora na kupima.

Amewataka washiriki kuyazingatia mafunzo ili wafanye kazi kwa uweledi na udalifu badala ya kufanya kazi kwa vitisho kama askari.

Aidha amewataka washiriki kujikita katika kutoa elimu kwa wadau ili kuboresha utendaji wa kila siku.

Mafunzo hayo yatakwenda sambamba na utoaji wa vishikwambi kwa Halmashauri zote ili taarifa ziweze kupatikana kwa wakati makao makuu ya Wilaya,Mkoa na Taifa.

"Niwatake washiriki mkayatumie mafunzo haya mliyoyapata kuleta mabadiliko chanya kwa Shirika na Taifa kwa ujumla"alisema Dkt Ashura.

Akiwahutubia washiriki katika ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya Mwajabu Mkomola amesema mafunzo yamekuja kwa wakati ili kuleta ufanisi katika shirika na serikali kwa ujumla.

Hata hivyo amesema mafunzo hayo yamemjengea uwezo wa kuelewa sheria mpya hasa baada ya kitenganishwa majukumu ya kiutendaji baina ya TMDA na TBS.

Sambamba na elimu ya mgawanyo wa Mapato(Ada na Tozo),Mgawanyo wa utekelezaji wa madaraka na majukumu yaliyoshirikishwa.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Washiriki Afisa Biashara wa Mkoa wa Mbeya Richard Musingi Salegote amesema kiu yao ni kupata mafunzo ambayo yatawajengea uadilifu katika utendaji wa kila siku.Amesema vishikwambi walivyovipata watavitumia ili kuyafikia malengo yaliyokusudiwa.

Mafunzo haya yanafanyika nchini kote yakihusisha sekta ya Afya na Biashara yakienda sambamba na utoaji wa vishikwambi.

                                                                             MWISHO