TPSF kufanya mkutano mkubwa Jijini Dar es Salaam.
Taasisi ya sekta binafsi nchini(TPSF)kwa kushirikiana na vyama vya wafanyabiashara na Wizara ya Viwanda uwekezaji na biashara imeandaa siku ya sekta binafsi itakayofanyika disemba 2,2022 katika ukumbi wa Super Doll Masaki Jijini Dar es Salaam ambapo watu zaidi ya elfu moja kutoka sekta za kiuchumi watashiriki.
Lengo ni kutoa shukurani pia kutambua mchango mkubwa wa sekta binafsi na mazingira rafiki katika kukuza uchumi wa Taifa letu chini ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.
Miongoni mwa washiriki ni pamoja Mawaziri, wakurugenzi na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali.

0 Comments
Post a Comment