*TANZIA*
*Anaandika Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mh.Siriel Mchembe*ππΏππΏππΏππΏππΏ
Niimepokea taarifa kutoka kwa *DC Rungwe Dkt. Vincent Anney* kwamba alfajiri ya leo, Hakimu *Joakim Mwakyolo* wa Mahakama ya Wilaya hapa Handeni ameuawa na wananchi wenye hasira kali huko Busokelo Tukuyu/Rungwe.
Marehemu alikuwa likizo maana huko Rungwe ndipo anapotokea.
Chanzo cha kuuawa ni Mgogoro wa Ardhi kati yake na wanakijiji hicho anachotoka.
Alishindwa kesi ya ardhi Mahakama Kuu dhidi ya kijiji, lakini baada ya muda akaonekana kwenye eneo la Mgogoro akiwa ameongozana na Watu wawili.
Inadaiwa kuwa yeye na watu hao wawili kuna vitu walikuwa wanavichimbia ardhini kwenye eneo hilo la mgogoro jambo ambalo lilitafsiriwa na wanakijiji kwamba ni ushirikina.
Wananchi walipowazonga watatu hao na kuwahoji kuhusu suala hilo, ugomvi ukatokea kati yao, jambo lililopelekea mmoja wa watu waliokuwa na Hakimu huyo kuwapiga risasi wanakijiji wawili miguuni.
Baada ya hapo wananchi wakapandwa hasira na kumshambulia kwa mawe na silaha mbalimbali Hakimu huyo pamoja mmoja wa watu aliokuwa nao, huku mwingine akitoweka kuelekea kusikojulikana.
Hivyo vifo vilivyoripotiwa ni viwili. Hakimu pamoja na mmoja wa watu alikwenda nao kwenye eneo la mgogoro.
Pole sana Mhimili wetu wa Mahakama, hasa Hakimu wa Wilaya Handeni Mhe.Sabuni kwa kuondokewa na mtumishi huyu.Poleni ndugu zangu wa Handeni.

0 Comments
Post a Comment