Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amezindua Jukwaa la Wadau na kufungua kikao cha kwanza cha Kamisheni ya pamoja ya Bonde la Mto Songwe unaojumuisha nchi za Tanzania na Malawi.

Katika hotuba yake ya ufunguzi amebainisha Bonde la mto Songwe lenye ukubwa wa kilometa elfu nne mia mbili arobaini na tatu linajumuisha Wilaya saba,tano za Tanzania ambazo ni Kyela,Mbeya Vijijini,Ileje,Mbozi na Momba na Wilaya mbili za Malawi ni Karonga na Chitipa ambazo hunufaika na maji kwa ajili ya matumizi ya majumbani na umwagiliaji ambapo matarajio ni kufungua mradi mkubwa wa uzalishaji umeme utaongiza kwenye gridi za Taifa kwa nchi hizo mbili.

Mahundi amesema suala kubwa na ambalo pia ameomba kuweka msisitizo ni kuwa”ukiwa mjumbe katika Jukwaa hili,usiulize Jukwaa litakupa nini,ila ujiulize utalisaidiaje Jukwaa katika kufanikisha malengo yake”alisema Mahundi.
Pamela Temu Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Raslimali za Maji Tanzania anaeleza lengo la kikao hicho cha kwanza kilichofanyika Jijini Mbeya ni kubadilishana uwezo na kuunganisha nguvu na rasilimali fedha na kutafuta vyanzo vyake ili kutekeleza mradi huo wa Bonde la Mto Songwe.

Aidha Mhandisi Elice Englibet Mkurugenzi wa Bodi ya Maji ya Bonde la Ziwa Nyasa na mwenyeji wa mkutano anaeleza faida na changamoto za mto huo amesema kuhamahama kwa mto Songwe ni kuhamahama ambapo husababisha mafuriko.

NAIBU WAZIRI WA MAJI AMEZINDUA JUKWAA LA WADAU NA KUFUNGUA KIKAO CHA KWANZA CHA KAMISHENI YA PAMOJA YA BONDE LA MTO SONGWE JIJINI MBEYA

Kujengwa kwa mabwawa kutapunguza kuhamahama kwa mto Songwe na kuwaondolea hofu kwani miaka ya nyuma baadhi walipoteza maisha na kupoteza mali nyingi hivyo Jukwaa hili litakuwa na manufaa makubwa kwa nchi zoe mbili.

Awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa umeanza ujenzi wa bwawa ambalo litazalisha umeme na ajira wakati awamu ya pili itajenga huduma za afya,miundombinu na elimu.