WAZIRI MKUU MAJALIWA ASHUHUDIA
RUWASA YASAINI MRADI WA MAJI WA VIJIJI 56 VYA RUANGWA NA NACHINGWEA.

Wizara ya Maji kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) imesaini mradi mkubwa wa maji wa Nyangao
- Ruangwa - Nachingwea utakaowezesha kufikia lengo la kitaifa la upatikanaji wa huduma ya maji vijijini kwa zaidi ya asilimia 85.

Mradi huu, unajumuisha vijiji 34 vipo Wilaya ya Ruangwa, vijiji 21 vipo Wilaya ya Nachingwea na Kijiji kimoja katika Wilaya ya
Lindi vyenye wakazi wanaokadiriwa kufikia 128,657.

Chanzo cha mradi huu ni Mito Nyangao a Chiue iliyopo Wilaya ya Lindi. Kwa pamoja chanzo kitakuwa na uwezo wa kuzalisha maji wastani wa lita 15,000,000 kwa siku, wakati mahitaji ya maji kwa vijiji vote vilivyopangwa kuhudumiwa na mradi huu kwa miaka 20 ijayo ni wastani wa lita 6,912,000 kwa siku.

Ili mradi ukamilike kwa wakati, mradi huu umegawanywa katika sehemu (Lots) mbili, ambapo kila sehemu itakuwa na mkandarasi wake.

Sehemu ya kwanza itahusisha ujenzi wa dakio la maji, ujenzi wa bomba kuu la maji mtiririko (gravity main) na maji ya msukumo (pumping main) jumla ya km 85 yenye ukubwa wa kipenyo cha mm 500. Sehemu hit itatekelezwa na Kampuni ya STC Construction Company Limited ya Dar Es Salaam kwa gharama ya Sh. 12,417,026,276.92 bila Kodi ya Ongezeko la
Thamani kwa muda wa miezi kumi nan ne (14).

Sehemu ya pili inayohusisha kazi zote zilizobaki, itatekelezwa na Mkandarasi Emirate Builders Co. Limited ya DarEs Salaam kwa Sh. 107,138,897,161.00 bila Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa muda wa miezi ishirini na sita (26). Kampuni zote mbili ni za Kitanzania.