Mtandao wa Kijinsia TGNP Mtandao umeendesha warsha kwa Watumishi wa Halmashauri ya Mbeya wakiwemo maafisa elimu,maafisa maendeleo ya jamii, madiwani na watendaji lengo ni kuwajegea uwezo wa kusimamia bajeti yenye mrengo wa Kijinsia warsha iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya Mwalingo Kisemba katika ukumbi wa Halmashauri eneo la Iwindi.Anna Sangai ni Afisa Program Mafunzo TGNP Mtandao amesema lengo la warsha ni kuwajengea uwezo watendaji hao ili waweze kuelewa namna ya kuandaa bajeti yenye mrengo wa Kijinsia hususani elimu, afya na miundombinu.
Naye Deogratius Temba kutoka TGNP Mtandao amesema awali wanawake wengi wa pembezoni walikuwa hawezi kujiamini pia kutogombea nafasi za kiuongozi lakini baada ya kupata elimu hivi sasa wengi wanajitokeza kugombea.
TGNP MTANDAO YAWAJENGEA UWEZO WATUMISHI WA HALMASHAURI WILAYA YA MBEYA.
Mtandao wa Kijinsia TGNP Mtandao umeendesha warsha kwa Watumishi wa Halmashauri ya Mbeya wakiwemo maafisa elimu,maafisa maendeleo ya jamii, madiwani na watendaji lengo ni kuwajegea uwezo wa kusimamia bajeti yenye mrengo wa Kijinsia warsha iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mbeya Mwalingo Kisemba katika ukumbi wa Halmashauri eneo la Iwindi.
Mwalingo Kisemba amesema Halmashauri yake imefanya kazi na TGNP Mtandao zaidi ya miaka kumi na katika muda huo wameshirikiana kufanya mambo mengi ikiwemo utengenezaji wa bajeti kwa zjili ya taulo za kike na Halmashauri yake ni miongoni mwa Halmashauri zinazofanya vizuri.
Anna Sangai ni Afisa Program Mafunzo TGNP Mtandao amesema lengo la warsha ni kuwajengea uwezo watendaji hao ili waweze kuelewa namna ya kuandaa bajeti yenye mrengo wa Kijinsia hususani elimu, afya na miundombinu.
Katika hatua nyingine viongozi hao watoe elimu kwenye jamii namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake sambamba na kukamilisha ushahidi katika kesi.
Naye Deogratius Temba kutoka TGNP Mtandao amesema awali wanawake wengi wa pembezoni walikuwa hawezi kujiamini pia kutogombea nafasi za kiuongozi lakini baada ya kupata elimu hivi sasa wengi wanajitokeza kugombea.
Amesema kwa sasa jamii imeunda vikundi vya taarifa na maarifa ambavyo vimesaidia kutoa taarifa ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake sambamba na kuwafikisha watuhumiwa kwenye vyombo vya sheria.
Agnes Elikunda Mkuu wa idara ya maendeleo ya jamii Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya amesema Halmashauri imetenga bajeti kwa ajili ya shule za msingi na sekondari na wamezidi kuongeza bajeti kila mwaka.
Emiana Mbise Afisa ustawi wa jamii Wilaya ya Mbeya amesema elimu waliyoipata itasaidia kuleta chachu katika jamii ingawa idara yake inakabiliwa na ukosefu wa fedha za kuwasaidia watu waliokumbwa na kadhia.
Afisa elimu sekondari Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya Lugano Malakasuka amesema elimu waliyoipata itawasaidia sana kwenye jamii hususani wanafunzi.
Naye Diwani wa Kata ya Ijombe Mary Mbengale amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya imeendesha mafunzo mbalimbali kwa madiwani namna ya kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake hususani ulawiti kwa watoto wa kike na kiume
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Mshewe Boniphace Njema amesema hivi sasa elimu itolewe kwa watoto hasa kukabiliana na vitendo vya ushoga ambavyo vimeanza kujitokeza nchini.
"Isiwe kutoa elimu tu bali sasa tuvikemee vitendo hivyo kwa nguvu zote"alisema Diwani Njema.
Tangu TGNP Mtandao kuanza kutoa elimu ya Kijinsia katika Wilaya ya Mbeya kwa zaidi ya miaka kumi Wanawake wengi wamekuwa wakijiamini zaidi kugombea nafasi za kiuongozi sambamba na kuunda vikundi vya taarifa na maarifa ambapo vitendo vya ukatili dhidi ya watoto na wanawake vimekuwa vikifichuliwa.
0 Comments
Post a Comment