*NAIBU WAZIRI WA MAJI MHE. MARYPRISCA W. MAHUNDI (MB), ASHUHUDIA MAKABIDHIANO YA MRADI WA BWAWA HANDENI.*
Leo Tarehe 14 Julai, 2023.Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi amekuwa mgeni rasmi kwenye Hafla ya makabidhiano ya mradi wa Bwawa la Maji la Kwamaizi kati ya Kampuni ya bia ya Serengeti (SBL) na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Handeni (HTM).
Bwawa hilo limejengwa kwa gharama ya shilingi milioni 419 ambapo umetekelezwa kwa ushirikiano kati ya Kampuni ya SBL na Taasisi ya Water Aid.
Utekelezaji wa mradi huo ulihusisha pia usanifu na ujenzi ambapo Bwawa hilo lina ujazo wa zaidi ya mita za ujazo 137,000 na lina uwezo wa kuwanufaisha wananchi zaidi ya 2,000.
Naibu Waziri wa Maji ameipongeze kampuni ya bia ya Serengeti na taasisi ya WaterAid kwa kushirikiana kupeleka Maji Safi na Salama kwa wananchi.
Amesema taasisi hizo zimekamilisha ujenzi wa mradi huo ndani ya miezi mitano ambapo pia amewapokeza RUWASA Mkoa na MD- HTM kutokana na usimamizi mzuri wa mradi.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe. Adv Albert Msando, Mbunge wa Jimbo la Handeni Mjini Mhe. Reuban Kwagilwa, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, wadau wa sekta ya maji pamoja na wananchi.
0 Comments
Post a Comment