Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Maryprisca Mahundi ameendelea kuambatana na Mwenyekiti UWT TAIFA kwa ajili ya Ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi 

Wakati wa Ziara hiyo, Mwenyekiti wa UWT TAIFA ametembelea na kukagua shule ya Sekondari ya wasichana Kilangala ambapo Naibu Waziri wa Maji ametolea ufafanuzi wa huduma ya kuboresha huduma ya maji katika shule hiyo kwa kutoa maagizo kwa RUWASA Mkoa wa Lindi kuwa ndani ya Wiki Mbili wakamilishe Ulazaji wa Mtandao wa mabomba wenye urefu wa Kilomita *19* ili kuhakikisha shule hiyo inapata huduma ya maji kwa muda wote.




*Shule ya Wasichana ya Lindi- Kilangala kupata huduma ya* *maji kabla ya tarehe 5 Agosti, 2023* 
*
18 Julai, 2023 ( Mchinga)


Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Maryprisca Mahundi ameendelea kuambatana na Mwenyekiti UWT TAIFA kwa ajili ya Ziara ya kukagua utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi 

Wakati wa Ziara hiyo, Mwenyekiti wa UWT TAIFA ametembelea na kukagua shule ya Sekondari ya wasichana Kilangala ambapo Naibu Waziri wa Maji  ametolea ufafanuzi wa huduma ya kuboresha huduma ya  maji katika shule hiyo kwa kutoa maagizo kwa RUWASA Mkoa wa Lindi kuwa ndani ya Wiki Mbili wakamilishe Ulazaji wa Mtandao wa mabomba wenye urefu wa Kilomita *19* ili kuhakikisha shule hiyo inapata huduma ya maji kwa muda wote.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa UWT TAIFA Ndugu Mary Pius Chatanda amefurahishwa kwa jitihada hizo na kusema kuwa Wizara ya Maji ikiahadi  inatekeleza.

Vilevile, Naibu Waziri wa Maji ameeleza  kuwa Serikali inaendelea na utekelezaji wa mradi wa usambazaji maji kutoka Mjini Lindi hadi Mchinga kwa gharama ya *Bilioni 13*