WAKANDARASI WATAKIWA KUTUMIA

BILIONI 7.2 ZA UJENZI WA MIRADI YA MAJI KWA WELEDI NA

KUZINGATIA MUDA.


Nimewataka wakandarasi wa miradi yam aji, waliopewa

dhamana ya kutekeleza miradi ya maji mkoani Arusha, kufanya

kazi hiyo kwa weledi na wakati. Serikali imehakikisha fedha

inapatikana ili wananchi wapate huduma ya majisafi, hivyo

weledi na ubora wa miradi yam aji katika utekelezaji ni jambo la

msingi.


Nimesema hayo wakati wa utiaji Saini wa mikataba ya ujenzi

wa miradi ya maji katika wilaya nne mkoani Arusha. Jumla ya

miradi ya maji minne yenye thamani ya takribani shilingi bilion

7.2 imesaini katika hafla hiyo kwa ajili ya ujenzi na usanifu wa

uboreshaji wa maji vijijini katika Wilaya za Ngorongoro; Karatu;

Arumeru; na Monduli Mkoani Arusha.


Akiwasilisha taarifa Mhandisi Joseph Makaidi kutoka Wakala

ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) amesema

miradi hiyo minne ina thamani ya shilingi bilion 7.2. Amesema

kwamba miradi hiyo ni mradi wa Maji Pori Tengefu la Pololeti

wilayani Ngorongoro awamu ya pili pia ujenzi wa mradi wa maji

Uwiro Wilaya ya Arumeru, mradi wa Endonyawet na Matala

Wilaya ya Karatu.


Mhandisi Makaidi amesema mradi wa Pololeti unatekelezwa

kwa thamani ya shilingi bilion 3.553 na Mkandarasi Jandu

plumber, mradi wa Uwiro wilayani Arumeru unatekelezwa na

Mandarasi Gopa kwa thamani ya shilingi bilion 1.887,

Mkandarasi kampuni ya Climax mradi katika Wilaya ya Karatu

kwenye Kata za Endonyawet na Matala kwa thamani ya million

839.618 na Mkandarasi mshauri wenye thamani ya takribani

shilingi bilion 4.


Awali akiongea kwenye hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Arusha

John Mongela Amesema kwamba zaidi ya shilingi bilioni 800

zimetolewa katika mkoa wa Arusha kwa ajili ya utekelezaji wa

miradi ya maji.


 Amesema utekelezaji wa miradi ya maji mkoa

wa Arusha unaenda kufikia lengo la asilimia 85 vijijini, na

katika bajeti miradi 26 imetengewa fedha na inaenda

kutekelezwa.