Akizungumza na waandishi wa habari, Kiongozi wa Msafara akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Lazaro Mboma, amesema kuwa Hospitali imepata fursa ya kushiriki maonyesho hayo ili ktangaza huduma za kibingwa zaidi ili kuweza kuleta wagonjwa wao kwa kupata matibabu kwa ufanisi zaidi badala ya kwenda mataifa ya mbali kwani Tanzania inatumia teknolojia ya hali ya juu katika matibabu
 

Amesema, Hospitali Rufaa ya Kanda Mbeya inasifika kwa vifaa vya kisasa na wataalamu wa matibabu waliobobea, inatarajia kuvutia wageni wengi zaidi katika lango kuu la kiuchumi katika nchi zilizoko Kusini mwa jangwa la Sahara SADC kwa kuangazia ubora wa huduma za afya zinazopatikana




HOSPITALI YA RUFAA YA KANDA MBEYA WAPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA NCHINI ZAMBIA

Katika azma ya kutangaza tiba utalii(medical Toursim) kitaifa na kimataifa, Wataalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya wanashiriki katika maonesho ya 95 ya kilimo na biashara Lusaka Zambia ambayo ni moja ya nchi Wanachama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuanzia ya tarehe 02 hadi 07 Agosti 2023.


Akizungumza na waandishi wa habari, Kiongozi wa Msafara akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya, Dkt. Lazaro Mboma, amesema kuwa Hospitali imepata fursa ya kushiriki maonyesho hayo ili ktangaza huduma za kibingwa  zaidi ili kuweza kuleta wagonjwa wao kwa kupata matibabu kwa ufanisi zaidi badala ya kwenda mataifa ya mbali kwani Tanzania inatumia teknolojia ya hali ya juu katika matibabu


Amesema, Hospitali Rufaa ya Kanda Mbeya inasifika kwa vifaa vya kisasa na wataalamu wa matibabu waliobobea, inatarajia kuvutia wageni wengi zaidi katika lango kuu la kiuchumi katika nchi zilizoko Kusini mwa jangwa la Sahara SADC kwa kuangazia ubora wa huduma za afya zinazopatikana. 

Dkt Mboma ameeleza kuwa mpango huu ni sehemu ya kampeni pana yakukutana na wadau kutoka nchi mbalimbali zilizohudhuria ili kutangaza teknolojia ya kisasa katika sekta ya afya mkoani Mbeya na maeneo jirani, na unatarajiwa kuwa na matokeo chanya katika uchumi wa ndani ambapo nchi ya Tanzania kwa uzuri wake wa asili na urithi tajiri wa kitamaduni, Mbeya inakuwa mahali pa lazima kutembelewa na wasafiri kutoka kote ulimwenguni.


Aidha, Dkt. Mboma ameongeza kuwa Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya itaendelea kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wa Tanzania na nchi Wanachama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pia kuwa tayari kushirikiana na nchi nyingine katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi.


Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya inatoa huduma za kibingwa na vipimo mbalimbali zikiwemo huduma za upasuaji wa kibingwa kama vile upasuaji wa moyo, ubongo na uti wa mgongo, figo, ini, upasuaji wa wadogo na matibabu ya saratani, huduma za magonjwa ya akili na matibabu ya kisaikolojia, huduma za magonjwa ya wanawake kama vile matibabu ya uzazi na matibabu ya magonjwa ya kizazi, huduma za upasuaji wa mifupa na mishipa ya damu, huduma za magonjwa ya kisukari na magonjwa ya figo.