Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametembelea na kukagua mradi wa usambazaji maji kutoka Makongo had Bagamoyo uliotekelezea na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dares salaam (DAWASA) katika kata ya Mivumoni na kuridhishwa na kazi iliyofanyika kuwafikishia wananchi huduma ya maji.
Nikiri kuwa Wilaya ya Kinondoni hapo awali ilikua na changamoto kubwa ya maji hasa eneo hili la Mivumoni lakini kwa sasa maeneo mengi wanapata huduma ya maji kwa saa
24 ."

"Nipende kumshukuru Mh. Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kwa kazi kubwa anayoifanya katika sekta ya maji, mradi huu ni mfano wa mapinduzi makubwa katika sekta ya maji nchini.
Nikiri kuwa Wilaya ya Kinondoni hapo awali ilikua na changamoto kubwa ya maji hasa eneo hili la Mivumoni lakini kwa sasa maeneo mengi wanapata huduma ya maji kwa saa
24 ."ameeleza Mheshimiwa Maryprisca.
Ameongeza kuwa huduma bora ya maji kama ilivyoboreshwa katika Wilaya ya Kinondoni ndio dhamira ya Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani kwa vitendo na ndio dhamira ya Wizara ya Maji kuna kila eneo huduma ya maji inafika.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambule amepongeza kazi kubwa iliyofanywa na DAWASA katika utekelezaji wa mradi huo na kumhakikishia Mhe Naibu Waziri kuwa malalamiko ya Maji yanakwisha Wilaya ya Kinondoni yamekwisha.
"Maeneo machache ambapo makazi Maya yanaendelea kujengwa tunaamini kuwa huduma itafika kwa wakati, kwa sasa kazi ya maunganisho ya maji inaendelea na kila kaya itapata huduma ya maji" ameeleza Mh.Mtambule
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji maji DAWASA, ambaye pia ni kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Mhandisi Shaban Mkwanywe amemshukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kwa kwa kuidhinisha fedha za utekelezaji wa mradi huo zaidi ya Tsh Bilion 65 zilizoenda kumaliza kilio cha upatikanaji wa huduma kwa wilaya tatu ambazo zimenufaika na mradi huu ambazo ni Wilaya ya Kinondoni, Ubungo na Bagamoyo.
0 Comments
Post a Comment