RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hasaan, ameipongeza Benki ya NMB kutokana na mchango wake kuinua Sekta ya Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na Misitu.

Dkt Samia amesema sapoti ya NMB kwenye Program ya Kuandaa Vijana na Wanawake Kujenga Kesho Iliyo Bora (BBT), imechangia kuboresha mchango wa kilimo ambapo ameshauri kushusha riba ya mikopo kwenye sekta hizo muhimu kwa nia ya kukuza uchumi wa Taifa.

Rais Samia Aipongeza  Benki ya NMB kuchangia Sekta ya Kilimo, BBT.

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hasaan, ameipongeza Benki ya NMB kutokana na mchango wake kuinua Sekta ya Kilimo, Uvuvi, Ufugaji na Misitu.

Dkt Samia  amesema sapoti ya NMB kwenye Program ya Kuandaa Vijana na Wanawake Kujenga Kesho Iliyo Bora (BBT), imechangia kuboresha mchango wa kilimo ambapo ameshauri kushusha  riba ya mikopo kwenye sekta hizo muhimu kwa nia ya kukuza uchumi wa Taifa.

Rais Samia ametoa pongezi na ushauri huo Jumatano Agosti 8, alipotembelea Banda la Benki ya NMB kwenye kilele cha  Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo Tanzania (Nane Nane 2023),yanayofanyika Jijini Mbeya.

Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Kilimo Biashara wa NMB, AgriBiashara Nsolo Mlozi,  akitoa taarifa mbele ya Rais Samia amesema  Sekta ya Kilimo (inayojumuisha kilimo chenyewe, Uvuvi, mifugo na misitu, benki yake imetoa mikopo ya zaidi ya Shilingi Bilioni 319 tangu Julai 2021 walipoanza kutoa mikopo kwa riba ya asilimia 9 kwa mwaka.

Mlozi amesema tangu mwezi March Benki ya NMB imetenga Tsh Bilioni 20 na program ya BBT. 

Kadhalika amesema Benki ya NMB inatoa  Elimu katika Vituo Atamizi kwa vijana na wanawake, ambao wamebeba kaulimbiu ya maonesho ya Kilimo ambapo Benki hiyo imedhamini kwa kutoa  Sh. Milioni 80.

Mlozi amemueleza Rais Samia kuwa, Benki ya NMB imetenga Sh. Bilioni 20 za mikopo ya ujenzi maghala ili kupunguza changamoto ya uharibifu na upotevu wa mazao na kuathiri thamani na ubora wake.  mazao ambapo pia wamekuwa na ushirikiano na Taasisi ya Agricom Africa wanaotoa Power Tillers na Matrekta na zana zingine za kilimo.