Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Ramadhani Kailima akizungumza leo Agosti 5,2023 wakati akitoa taarifa uwepo wa Uchaguzi mdogo katika Jimbo la Mbarali Mkoani Mbeya na Kata sita za Tanzania bara. Taarifa hiyo ameitoa jijini Dodoma baada ya kikao cha Tume kilichokutana leo . Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mh. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele (katikati) akiongoza kikao cha Tume kilichokutana leo Agosti 5,2023 jijini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Tume, Jaji wa Rufaa (Mstaafu), Mbarouk Salim Mbarouk na Kulia Katibu wa Tume hiyo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Uchaguzi wa tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhani Kailima.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiendelea na kikao chao hii leo Agosti 5,2023 jijini Dodoma.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiendelea na kikao chao hii leo Agosti 5,2023 jijini Dodoma.
Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiendelea na kikao chao hii leo Agosti 5,2023 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mh. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele (wanne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi baada ya kumalizika kwa kikao chao kilichokutana leo jijini Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine walipitisha tarehe ya uchaguzi mdogo katika jimbo la mbarali na Kata sita za Tanzania bara.
**********
Uchaguzi
Mdogo wa Jimbo la Mbarali na kata sita za Tanzania Bara utafanyika tarehe 19
Septemba, 2023.
Akisoma
taarifa kwa umma jijini Dodoma leo tarehe 05 Agosti, 2023, baada ya kikao cha Tume, Mkurugenzi wa
Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Bw. Ramadhani Kailima amesema wagombea
watachukua fomu kuanzia tarehe 13 hadi 19 Agosti, 2023, siku ya uteuzi itakuwa
tarehe 19 Agosti, 2023 na kampeni za uchaguzi zitafanyika kuanzia tarehe 20
Agosti, 2023 hadi tarehe 18 Septemba, 2023.
Amezitaja
kata zitakazofanya uchaguzi mdogo kuwa ni; Nala iliyopo Halmashauri ya Jiji la
Dodoma, mkoani Dodoma, Mwaniko iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi,
mkoani Mwanza, Old Moshi Magharibi iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi na
Marangu Kitowo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro,
Mtyangimbole iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na Mfaranyaki iliyopo Halmashauri
ya Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.
“Tume
inatumia nafasi hii kuvikumbusha vyama vya siasa, wagombea na wadau wote wa
uchaguzi kuzingatia Katiba, Sheria, Kanuni, Maadili ya Uchaguzi, Taratibu,
Miongozo na maelekezo ya Tume katika kipindi cha uchaguzi huu mdogo,” amesema
Bw. Kailima.
Aliongeza
kuwa, Tume imetoa taarifa hiyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiitaarifu Tume kuhusu uwepo wa
nafasi wazi ya Ubunge katika Jimbo la Mbarali, Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali
Mkoa wa Mbeya. Nafasi hiyo wazi
inatokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mhe. Francis Mtega. Spika ametoa taarifa hiyo kwa mujibu wa
kifungu cha 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343.
Aliongeza, “Tume
kwa kuzingatia matakwa ya kifungu cha 37(1)(b) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,
Sura ya 343 na kifungu cha 13(3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa,
Sura ya 292 inatoa taarifa kwa umma kuhusu uwepo wa uchaguzi mdogo wa Ubunge wa
Jimbo la Mbarali na Madiwani katika kata sita za Tanzania Bara”.
0 Comments
Post a Comment