November 26, 2020 Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dr. Tulia Ackson kupitia taasisi yake ya Tulia Trust amekabidhi mkopo wa pikipiki tano zenye thamani ya Tsh: 12,000,000/- kwa madereva bodaboda wa kata ya Iziwa Wilaya ya Mbeya mjini kwa lengo la kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi.

Dr. Tulia amesema>>>”Mara ya mwisho nilipokuja hapa nilikuwa nimekuja kuomba kura na nikaahidi kwamba tutafanya kazi, sasa leo sio siku ya kampeni tena bali tumekuja kuanza kutekeleza ahadi zetu ikiwemo ya kufanya kazi na vijana na tayari tumeshaanza. Leo tunaanza kwa kuwawezesha kwa kuwapatia hizi pikipiki tano na tutaendelea kuwawezesha kadri tuwezavyo”- Dr. Tulia Ackson


“Lakini pia hapa nimewaona vijana wengine ambao wao sio bodaboda, hawa wanafanya biashara nyingine na sisi tupo tayari kuwawezesha na tutafanya hivyo ili kuwasaidia kujiwezesha kiuchumi. Nimewaona pia wakinamama hapa wanajishughulisha na biashara, kupitia taasisi yetu ya Tulia Trust tutawapatia mikopo ili mfanikishe biashara zenu”- Dr. Tulia Ackson


“Baada ya kuzungumza haya ya kuhusu uwezeshaji naomba nimalizie kwa jambo moja, tunatamani Wananchi wa Mbeya mjini wote wawe na bima ya afya. Sisi tumejitolea kwa kaya maskini kuwalipia bima lakini upo mfumo mwingine kwa wale wanaojiweza kwa kulipa bima ya afya kwa Tsh: 30,000/- tu kwa mwaka mzima na unatibiwa wewe kama ni mke au mume pamoja na watoto wenu wanne”-Dr. Tulia Ackson