Kamishna wa Ubia kati ya Serikali na Taasisi Binafsi Dkt John Mboya akizungumza kwenye mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Kampasi ya Mbeya.
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Profesa  Carolyne Nombo akizungumza wakati wa Mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu Kampasi ya Mbeya.
Meneja wa TIA Kampasi ya Mbeya Mashaka Mbugi akizungumza kwenye Mahafali ya 18 ya Taasisi hiyo ambapo jumla ya Wanazuoni 1708 wamehitimu Vyeti na shahada
Kamishna wa Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi Dkt John Mboya (Kushoto) na Meneja wa Taasisi ya Uhasibu TIA Kampasi ya Mbeya Mashaka Mbugi(kulia) wakishiriki maandamano wakati wa mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu TIA Kampasi ya Mbeya.
Brass Band ya Jeshi la Magereza Kiwira Ikiongoza Maandamano kwenye Mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu TIA Kampasi ya Mbeya.

Baadhi ya Wanazuoni wa Taasisi ya Uhasibu TIA kwenye Mahafali ya 18 ya Taasisi hiyo Jijini Mbeya.



Mhitimu  wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Mbeya akipokea zawadi kwa kufanya vizuri masomo kutoka kwa Mgeni rasmi Kamishna wa Ubia kati ya Serikali na Taasisi Binafsi Dkt John Mboya mbele ya Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Profesa Carolyne Nombo wakifuatilia jambo kwenye mahafali ya 18 ya Taasisi hiyo Jijini Mbeya.

Ngoma aina ya Ling'oma ilinogesha mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu TIA Kampasi ya Mbeya.



Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Profesa Carolyne Nombo akiteta jambo na Meneja wa TIA Kampasi ya Mbeya Mashaka Mbugi wakati wa Mahafali ya 18 ya Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Mbeya
Burudani kwenye Mahafali ya 18 Taasisi ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Mbeya


MAHAFALI YA 18 TAASISI YA UHASIBU TIA KAMPASI YA MBEYA.

Jumla ya Wanazuoni 1,708 wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Kampasi ya Mbeya wamefanya mahafali ya kuhitimu mafunzo mbalimbali yanayotolewa Chuoni hapo.

Mgeni rasmi katika mahafali hayo Kamishna wa Ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi Dkt John Mboya amesema lengo la serikali katika elimu ni kuviwezesha vyuo kutoa mafunzo yenye tija kwa wahitimu ili waweze kujiajiri baada ya kuhitimu.

Hata hivyo Dkt Mboya amewataka wanazuoni na wanafunzi wa vyuo kutotumia ulaghai kwenye mitihani kwa kuwa kufanya hivyo watakuwa wamejiingiza katika hatia na kwamba kusoma kwa bidii na kufuata maelekezo wa walimu na wahadhiri ndio njia pekee itakayomsaidia mwanafunzi kufanya vyema katika mitihani yake.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Profesa Carolyne Nombo amesema Taasisi ya Uhasibu yenye matawi 6 nchini mbali na kutoa mafunzo kwa kozi mbalimbali imejikita katika kuihudumia jamii katika sekta za Elimu na Afya.

''Taasisi ya Uhasibu Kampasi ya Mbeya imeweza kufika katika shule za sekondari Iganzo,Iyunga na Samora ambako tumetoa elimu ya kuwahamasisha kujiunga na Taasisi yetu na kutoa misaada ya Vifaa vya Ujenzi na Madaftari''amesema Profesa Nombo.

Aidha Profesa Nombo amewataka wanazuoni wa TIA kuendelea kuipeperusha vyema bendera ya TIA huko waendako baada kuhitimu Taasisi ya Uhasibu na kwamba Taasisi hiyo imejikita kwenye mafunzo kwa kuongeza Udahili kwa kipindi cha mwaka 2019 -2020. 

Kwa upande wake Meneja wa Taasisi ya Uhasibu Kampasi ya Mbeya Mashaka Mbugi amesema wahitimu 1,708 waliopokea vyeti vyao wamepitia safari ndefu katika masomo yao na kwamba baada ya kutoka chuoni hapo wanatarajiwa kuongeza ajira kwa kujiajiri huko uraiani.