MELI YA MV MBEYA II IMEANZA RASMI SAFARI ZA KIWIRA HADI MBAMBA BAY, NYASA - RUVUMA.


Meli ya Abiria na Mizigo ya  Mv Mbeya II, Leo imetia nanga katika Bandari ya Mbamba bay Wilayani Nyasa na kuanza Rasmi safari zake kutoka Bandari ya Kiwira hadi Mbamba bay.


Meli hiyo imefika Mbamba bay saa 4 na nusu  Asubuhi, Ikiwa na abiria na mizigo, mbalimbali yakiwemo magari,  na kupokelewa kwa hamu na wakazi wa Mbamba bay Wilayani Hapa, na mara baada ya kutia Nanga wananch,i waliingia ndani ya meli kwa shauku kubwa na kufanya Utalii wa kupiga picha na kushangilia huku wakisema, Tunampongeza sana Rais John Pombe Magufuli kwa kuiweka katika ramani ya Maendeleo kwa kutatua kero ya Usafiri wa majini na Nchi kavu katika Wilaya ya Nyasa, ambao hapo awali haukuwepo.


Baadhi ya Abiria waliofika na meli hiyo, wakiongea mara baada ya Meli kuwasili Bw steven Mkomola amesema usafiri wa meli ni Mzuri sana yeye ametoka Dar es s,alaam akiwa na Gari yake Binafsi amepitia Bandari ya Kiwira, na amesafiri na Meli hiyo na amewashauri wananchi kutumia Usafiri wa majini Ziwa Nyasa kwa kuwa inakata Mawimbi na ina uwezo mkubwa.


Naye Claudeni Mwangosi amesema alikuwa anasafirisha gari lake toka Kyela hadi Mbamba bay na kufika salama kwa bei nafuu. Amesema Nyasa kumefunguka wageni wakaribie kuwekeza Nyasa. Na katika Picha waweza kuona sehemu mbali mbali za Meli hiyo.


Meli ya MV Mbeya II inafanya safari kutoka Kiwira hadi Mbamba bay, Nyasa - Ruvuma kila siku ya Jumatatu na kufika Mbamba bay siku ya Jumanne, na Kuondoka Mbamba Bay Jumatano na kufika Kiwira Alhamis kila Wiki.