•  Naibu waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Jerry Muro mara baada ya kufika ofisini kwake kujua namna ambavyo utekelezaji wa mradi mkubwa wa Maji utawanufaisha wakazi wa Wilaya hiyo.


 Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi yupo katika ziara mikoa ya Kaskazini ambako ametembelea wilayani Arumeru mkoani Arusha ili kujionea na kupata maelezo ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa Maji mkoani Arusha.


Akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mhandisi amekutana na Mkuu wa Wilaya hiyo Jerry Muro ambaye amemueleza mahitaji makubwa ya maji wilayani humo.


Naibu waziri Meyprica akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru yupo njiani kuelekea kwenye mradi mkubwa wa Maji wenye thamani ya Shilingi Bilioni 520 ambao utasaidia kupunguza ama kuondosha kabisa tatizo la Maji katika mkoa wa Arusha na wilaya ya Arumeru.