Naibu Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi, amesema Mradi wa Maji wa Pongwe uliopo wilaya ya  Mheza mkoani Tanga unaogharimu Sh. Bilioni 6.1 umefikia asilimia 75 na utakamilika Februari mwakani na hivyo kumaliza tatizo la mgao wa Maji kwenye Mji wa Mheza linalowakabili wananchi.