*WAZIRI WILLIAM LUKUVI AMALIZA MGOGORO WA ARDHI MJI MWEMA-CHANG'OMBE,AAMURU WANANCHI KUMILIKISHWA MAENEO*
Waziri wa Adhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi **Mh William Lukuvi **leo ametatua mgogoro wa ardhi katika Mtaa wa Mtakuja,Mji Mwema-Chang'ombe uliodumu kwa miaka mingi kwa kuamuru wananchi kutovunjiwa nyumba zao na kuondolewa na badala yake kurasimishiwa na kumilikishwa maeneo husika.
Mh Lukuvi ametoa maelekezo hayo leo katika mkutano wa hadhara wa wananchi uliofanyika mtaa wa Mtakuja ambapo alieleza kuwa ni dhamira ya *Mh Rais Dr.John Pombe Magufuli* kuhakikisha kwamba wananchi wote wanyonge wanatatuliwa changamoto zao hasa kwenye umiliki wa ardhi.
"Maagizo ya Mh Rais ni kwamba hakuna mwananchi atakayevunjiwa nyumba wala kuondolewa,wote mtarasimishiwa maeneo yenu na kupewa hati za umiliki na nataka zoezi hili likamilike ifikapo Februari mwishoni mwaka 2021"Alisema Mh Lukuvi.
Wakati huo huo,Mkuu wa Mkoa wa Dodoma *Dr.Binilith Mahenge* ameahidi kusimamia utekelezaji wa maelekezo hayo kwa kuhakikisha kwamba eneo hilo wananchi wanarasimishiwa na kupewa hati za umiliki.
Aidha akizungumza katika mkutano huo,Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini *Mh. Anthony Mavunde* ameishukuru serikali kwa maamuzi ya kulifanya eneo la Mtakuja kama eneo rasmi la makazi na hivyo kutatua mgogoro wa ardhi uliodumu kwa miaka mingi katika eneo hilo na kwamba kupitia hati milki za maeneo husika wananchi watapata fursa ya kuweza kukopa kwa ajili kuinua mitaji yao au kuanzisha shughuli za kiuchumi.
0 Comments
Post a Comment