Mkuu wa wilaya ya Chunya Mayeka Simon Mayeka, katikati akiwa ambatana na Waheshimiwa Wabunge, walipotembelea Maendeleo ya Ujenzi wa Daraja la mto Lupa Desember 2. 2020, Mwenye Suti Nyeusi ni Mhe. Masache Njelu Kasaka Mbunge jimbo la la Lupa na Mwenye Suti ya Kijivu ni Mhe. Maryprisca Mahundi Mbunge Viti Maalumu mkoa wa Mbeya.
Mkuu wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Mayeka Simon Mayeka akiongozana na Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Njelu Kasaka pia Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi wametembelea daraja la mto Lupa ili kukagua ujenzi unaoendelea katika barabara ya Chunya Makongolosi.
Lengo la kutembelea daraja hilo ni kusuasua kwa mkandarasi ambaye alipaswa kuimaliza barabara hiyo kwa mujibu wa mkataba baina yake na serikali.
Hata hivyo licha ya kuongezewa muda kuikamilisha barababara hiyo lakini bado kuna maeneo hayajakamilika kwa madai ya kuwepo kwa mvua nyingi kulikosabsbisha kusimama kwa mradi huo mara kwa mara.
Mkuu wa wilaya amemwagiza Mhandisi Ibrahim Joram wa Wakala wa barabara(TANROAD) kuanzia sasa waache kazi nyingine zote wajikite kwenye daraja hilo la Lupa kuhakikisha wanafanya kazi usiku na mchana.
Mayeka amesema daraja hilo ni muhimu kwani linasaidia sana uchumi wa Chunya pia kurahisisha usafiri Mikoa ya Tabora,Singida na Kigoma ambao hutumia barabara hiyo.
Kwa upande wake Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema mapema mwaka huu daraja la zamani lilisababisha maafa baada ya kipande cha daraja kukatika na kusababisha barabara kufungwa kutokana na kujaa maji hali iliyowafanya wananchi kukosa mawasiliano.
Aidha Mbunge wa Lupa Masache Kasaka amesema daraja hilo ni kiuongo kwa uchumi wa wananchi wake hasa waliopembezoni hasa katika msimu huu wa kilimo kwa ajili ya kusafirisha pembejeo za kilimo na mazao likiwemo zao kuu la tumbaku linalolimwa tarafa ya Kipembawe.
Lawena Nsonda ni mfanyabiashara wa Makongolosi amesema serikali imhimize mkandarasi kukamilisha daraja kwani likikamilika litapunguza kadhia ya kutumia muda mrefu kusafiri kufuata huduma Wilayani Chunya na Mbeya.
Diwani wa Kata ya Matundasi Kimo Choga ameishukuru serikali kwa ujenzi wa barabara hiyo ambayo sasa imeongeza thamani ya majengo kwani hivi sasa wananchi wanajenga nyumba bora na za kisasa.
0 Comments
Post a Comment