Naibu Waziri wa Maji aahidi wiki mbili wananchi Iwindi wapatiwe maji.


Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa wiki mbili kwa Wahandisi wa maji kuhakikisha miradi ya maji Mwampalala,Itimu pia Mwashiwawala na Iwindi inatoa maji kama ilivyokusudiwa.

Mahundi alitoa agizo hilo kwa Wahandisi wa Maji Mkoa na Wilaya ya Mbeya katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kata ya Iwindi ambapo licha ya kutolewa pesa na serikali miradi hiyo haifanyi kazi kwa zaidi ya miaka mitano.

Awali Diwani wa Kata ya Iwindi Mfisile Nswila alisema kilio cha muda mrefu kwa wananchi wake ni maji.

Kwa upande wake Mbunge wa Mbeya Vijijini Olan Njeza alisema suluhu ya kero ya maji Kata ya Iwindi ni kuunganishwa na Mamlakav ya Maji.

Naye Mhandisi wa maji Wilaya ya Mbeya alisema bado wanaendelea na ufuatiliaji wa miundo mbinu kuhakikisha maji yanapatikana.

Rejina Mdendemi alisema amefurahishwa na ujio wa Naibu Waziri wa maji kwani wanayo matumaini ya kuondokana na kadhia ya ukosefu wa maji.

Aidha Daud Kapusi alisema wataalamu waongeze bidii ili maji yapatikane katika Kata ya Iwindi na vitongoji vyake.