BILIONI 16 KUNUFAISHA VIJIJI VISIVYOKUWA NA MAJI SONGWE
SONGWE: Katika kuongeza asilimiaya
upatikanaji wa maji vijijini kutoka asilimia 73 hadi asilimia 100, Mkoa wa
Songwe umepata jumla ya Shilingi Bilioni16.4 ikiwa ni fedha za utekelezaji wa
mradi wa maji Vijijini za mpango maalumu wa Lipa kwa Matokeo PfoR utekelezaji
unaotarajia kuanza hivi karibuni.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe Brige. Gen
Nicodemus Mwangela amesema miradi ya Maji inapojengwa na kukamilika inaongeza
asilimia ya upatikanaji wa Maji kwa Wananchi Vijijini.
‘’Nitoe Wito kwa Jamii kutunza vyanzo
vya Maji na kuilinda Miradi ili Wananchi wapate Maji kwa muda mrefu,’’amesema
Mwangela.
Mhandisi Pambe amebainisha kuwa
RUWASA imejipanga kutekeleza miradi hiyo ndani ya miaka mitatu ili vijiji vyote
visivyokuwa na maji katika mkoa wa Songwe vianze kutoa maji.
0 Comments
Post a Comment