MHANDISI MARYPRISCA AHUTUBIA WANAKIJIJI KAZENGA CHATO ATOA ELIMU YA UTUNZAJI MIUNDO MBINU YA MAJI

Na Ripota wa Mbeya Yetu,Chato

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Maryprisca Mahundi amewataka wananchi wa kijiji cha Kazenga Wilaya ya Chato Mkoa wa Geita kutunza miundombinu ya maji ili iwe endelevu kwa vizazi vijavyo.

Mheshimiwa Mahundi ameongea hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kazenga  waliosimamisha msafara wake ili waweze kuishukuru serikali kwa kuwajali kwa kuwakarabatia miundombinu ya mradi wao wa maji ambao uliacha kutoa maji tangu mwaka 1988.

 “Tunafahamu mlikuwa na mradi wa siku nyingi ambao muda mrefu ulikuwa hautoi maji lakini sasa mradi umefufuliwa na umeanza kutoa maji, tunafahamu vituo vitatu vimeanza kutoa maji na baadhi ya maeneo bado hawajaanza kupata huduma hiyo, nataka kuwahakikishia hivi vituo ambavyo havijapatiwa huduma ya maji baada ya mwezi mmoja vitapata maji”, amesema Mhandisi Mahundi.