MASACHE KASAKA AWATEMBELEA WANANCHI ITUMBI AWASHUKURU AWATIA MOYO KUSAIDIA KUTATUA CHANGAMOTO HUDUMA ZA KIJAMII


Mbunge wa Jimbo la Lupa wilaya Chunya Mkoani Mbeya Mheshimiwa Masache Njelu Kasaka ameendelea na utaratibu wake wa kuwashukuru wapiga kura wake kwa kufanya mikutano ya hadhara katika kata ya Itumbi kata ya Matundasi.

Akiwa kijijini hapo Mheshimiwa Kasaka amekutana na makundi mbalimbali ya watu wakiwemo wachimbaji wadogo wadogo ambapo ameahidi kufuatilia kero zao ili ziweze kutatuliwa.



Amesema Kijiji cha Itumbi ni kati ya vijiji vyenye wachimbaji wengi wa dhahabu ambako kuna changamoto nyingi za huduma za kijamii ikiwemo afya na elimu ambapo kwa kutumia ushirikishwaji wa wadau atajitahidi changamoto hizo zitapungua.

Aidha amesisitiza wananchi na wachimbaji wadogo kuendelea kuiamini serikali ya awamu ya tano ya Dkt John Pombe Magufuli ambayo imedhamiria kwa dhati kusaidia wanyonge katika maeneo mbalimbali yenye changamoto.