HABARI NJEMA KWA WAKULIMA WA UFUTA WILAYA YA SONGWE

Baada ya taharuki ya muda mrefu juu ya tija kwa wakulima wa bei ya Ufuta wilayani Songwe mkoani Songwe hatimaye mnada mkubwa uliofanyika katika kijiji cha Chang’ombe kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani Bei ya ufuta imepanda hadi kufikia Sh 2,291 kwa Kg 1 kutoka Sh 1,300 kwa Kg 1 ya awali kwa soko la Mbalizi.



Katika mnada huo ambao umehudhuriwa na Mkuu wa wilaya ya Songwe Samwel Jeremiah amesema kuwa bei hiyo imefikia hatua hiyo baada ya wakulima kuukubali mfumo kupitia vyama vya Ushirika AMCOS.
Amesema kuwa AMCOS mbili zilipanga kufanyika kwa mnada huo katika kijiji cha Chang’ombe na kupatikana kwa bei ya juu ya Ufuta ya Sh 2,291 kwa Kg 1 badala ya bei ya awali ya mitaani ya Sh 1,300 Kg 1.
Jeremiah amewataka wakulima kuuza ufuta kwa bei ya mtandaoni kwa soko la Kimataifa bila wakulima kufahamiana ikiwa ni pamoja na kukusanya mazao yao ghalani ambako  huko kuna uwezekano mkubwa wa kupata bei nzuri kupitia soko la Kimataifa.
Amesisitiza kuwa soko la leo limeweka uchanganuzi mzuri wa wapi mkulima ataona kuna tija  ya kuuza mazao yake.