Akitoa taarifa Kijiji cha Kisale Kata ya Ipinda kwa viongozi hao Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Ezekiel Magehema amesema baadhi ya wananchi chakula kimeharibika, nyumba zao zimeboka pia mazao yamesombwa na maji hivyo wanawakati mgumu wa kujikimu ambapo baadhi wamehifadhiwa na ndugu zao.
Aidha amesema baadhi ya maeneo miundo mbinu ya umeme,maji na barabara imeharibiwa hivyo kuwapa wananchi wakati mgumu pia kuleta kadhia ya usafiri kutokana barabara kukatika ambapo serikali inaendelea kufanya tathini ili kuona msaada gani unahitajika hivyo aliwashukuru Naibu Spika,Naibu Waziri wa Maji na Mbunge kufika kwa haraka mbali ya kuwsfariji lakini wametoa msaada wa chakula kwa wahanga.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Suma Fyandomo amesema maafa hayo kwa wananchi walipewa taarifa na Mbunge wa Kyela Ally Jumbe Mlagila hivyo wameungana naye katika kipindi hiki kigumu kinachowakabili wananchi wake hivyo aliwataka wananchi kumuomba Mungu ili kuwaepusha na majanga.
Aidha Fyandomo amewaomba wananchi kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuiongoza nchi kwa uweledi pia aangalie namna ya kuisaidia Wilaya ya Kyela ambayo ipo hatarini kukumbwa na njaa kutokana na mazao kusombwa na maji.
Akikabidhi chakula kilichotolewa kilo mia sita hamsini za unga,kilo mia mbili arobaini za maharagwe na kilo mia mbili za mchele Naibu Spika Dkt Tulia Ackson amesema tukio hilo wamelipokea kwa masikitiko makubwa kupitia kwa Mbunge wa Kyela na alisema anafuatilia ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa ili kuona namna ya kuwasaidia wananchi wa Kyela..
Dkt Tulia amesema kaya nyingi zimeathiriwa na mafuriko ameshauri kipaumbele kiwe kwa wenye uhitaji mkubwa kwani wao wanafahamiana.
Amesema wamejionea hali halisi hivyo wataungana na Mbunge wa Kyela pindi atakapowasilisha hoja hiyo Bungeni katika vikao vinavyoendelea.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisale Jackson Mwakambulo amesema kuwawanaishukuru serikali kwa hatua ya haraka waliyoichukua ili kukabiliana na janga hilo.
"Nachukue fursa hii kuiomba serikali msaada wa mbegu zinazokomaa kwa muda mfupi ili tuweze kukabiliana na njaa"amesema Jackson.
Baadhi ya wananchi akiwemo Frola Lukuta na Hosea Mwankenja mbali ya kuishukuru serikali pia viongozi waliofika kutoa msaada wa chakula.
Ziara hiyo iliendelea Kijiji cha Mpunguti Kata ya Luteba ambapo Diwani wa Kata hiyo Ayub Mwalubona alisema mtu mmoja amefariki na nyumba ishirini na nane zimeanguka na miundo mbinu ya barabara na umeme imeharibika.
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi na Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Suma Fyandomo wamesema wameshtushwa na maafa hayo.
Naibu Spika Dkt Tulia Ackson amesema wameleta unga kilo 650 ,maharagwe kilo 240 na mchele kilo 200 ili zigawiwe familia zilizoathiriwa zaidi.
Mwenyekiti wa Kijiji Sadiki Mwakalukwa ameshukuru viongozi hao kwa kuwajali na kuwapa faraja.
0 Comments
Post a Comment