TAASISI YA LSF YATOA ELIMU YA MIKOPO MTAA
KWA MTAA
Na Mwandishi Wetu
Taasisi Isiyo ya Kiserikali LSF iliyo
chini ya Chuo Kikuu cha Teofilo Kisanji TEKU imeanza kutoa elimu kwa wananchi
katika vituo vya Mabasi ili kuwajengea uwezo wananchi kuepukana na mikopo umiza
inayotolewa na Taasisi zisizosajili rasmi.
Amesema kuwa mikopo hiyo
haishirikishi wenza kama vile mke na mume hivyo kusababisha migogoro katika
ndoa.
Kwa upande wake wakili Ezelina Mahenge
ambaye ni Mkufunzi wa mafunzo ya mikopo, amewaasa wananchi kubla ya kuingia
mikataba ya mikopo wanapaswa kusoma kwa makini mikataba na ikiwezekana
kuwatumia wanasheria katika vituo mbalimbali vilivyopo katika kila kata Jijini
Mbeya.
Ameiomba Taasisi kuendelea kutoa
elimu ili Wananchi wazidi kupata uelewa.
Zaidi ya wananchi laki mbili
wamefikiwa na Taasisi ya LSF kwa kipindi kisichozidi miezi 6 huku wengi
wakielewa namna ya kuanza kukopa mikopo yenye tija.
0 Comments
Post a Comment