TANZANIA NA
POLAND ZAKUBALIANA KUIMARISHA HUDUMA ZA MAJI SAFI NA USAFI WA MAZINGIRA MAJIJI
YA DAR NA DOM
Serikali ya
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Serikali ya Watu wa Poland zimeingia
makubaliano ya kuimarisha huduma za maji na usafi wa mazingira katika majiji ya
Dar es Salaam na Dodoma kupitia utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa miradi ya
maji Taka Mji wa Kiserikali na kuongeza kiwango cha upatikanaji maji Jijini Dodoma
na kupunguza upotevu wa maji Jijini Dar es salaam.Akizungumza
kwa Niaba ya Serikali ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Naibu Waziri
wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amesema kuwa hatua hii ni muhimu katika kuhakikisha Jiji la Dodoma
linafikia malengo kwa upatikanaji wa
maji ya Uhakika.Amesema kuwa
jambo hili limekuwa muhimu zaidi kutoka na umuhimu wake hasusan ikizingatiwa kuwa Jiji la Dodoma ndio makao
makuu ya nchi linalokuwa kwa kasi na ongezeko la watu na makazi.
Mhandisi
Mahundi amesema kuwa serikali imejizatiti barabara katika kukabiliana na
upotevu wa maji katika Jiji la Kibiashara la Dar e Salaam na kuongeza kiwango
cha makusanyo ya mapato na kudhibiti matumizi kupitia Mamlaka ya Maji Safi na
Usafi wa Mazingira(DAWASA).
Kwa upande
wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje anayesimamia Ushirikiano wa Kiuchumi na
Maendeleo ya Bara la Afrika na Afrika Mashariki ya Kati Mhe Pawel Jablonski
amesema serikali ya Poland ipo tayari kutekeleza makubaliano kwa lengo la
kuendeleza sekta ya maji nchini Tanzania na kuimarisha mahusiano ya nchi mbili
hizi.Kutoka Poland
ujumbe umeongozwa na Mhe Powel Jabionski Balozi wa Poland nchini Tanzania
Krzystol Buzailski na Maofisa Waandamizi kutoka nchini Poland.
Makubaliano
hayo ni matokeo ya majadiliano ya
takribani miaka mitatu tangu
serikali hizo zilipokutana kwa lengo la kukuzana kuimarisha ushirikiano kwenye
sekta ya maji nchini.
0 Comments
Post a Comment